
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa taarifa juu ya kasi ya mfumuko wa bei wa Taifa ambapo imesema, kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2023, umepungua kidogo hadi 4.8% kutoka 4.9% kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023.
.
Ofisi hiyo imesema kupungua kwa mfumuko huo kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Februari 2023.

