
Serikali imezindua kiwanda cha kutengeneza barakoa, aina ya N95, kilichopo katika Bohari ya Dawa iliyopo mkoani Dar es Salaam, ambazo zitasaidia kujikinga dhidi ya magonjwa ya hewa katika maeneo ya kutolea huduma za Afya.
.
Akizindua kiwanda hicho leo, machi 9, 2023, Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel, amesema matokeo hayo, ni kutokana na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, za kukuza uhusiano na mashirikiano na nchi mbalimbali, unaopelekea kuvutia uwekezaji katika eneo la viwanda.
