
Tanzania imeteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Advisory Body on Sport - CABOS) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2023 - 2025.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, imebainisha kuwa, hatua hiyo ni kutokana na kuimarika kwa nchi yetu katika nyanja za diplomasia ikiwemo michezo.

