
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, limekamata nyara mbalimbali za serikali ikiwemo meno ya tembo mazima 13 na vipande 13, jino moja la kiboko na miiba ya nungunungu.
.
Akitoa Taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Marco Chilya, amesema Jeshi hilo pia linawashikilia watuhumiwa watatu wa ujangili na silaha tatu zilizotumika kufanya ujangili.