
Wavuvi wawili katika Kijiji cha Mtandi kilichopo wilayani Mtwara, mkoani Mtwara, waliojulikana kwa majina ya Shani Salumu Yusuph (53) na Nangoma Salumu Yusuph(58), ndugu wa familia moja, wamefariki dunia, baada ya kupigwa na radi wakiwa kwenye shughuli za uvuvi katika Pwani ya Bahari ya Msimbati ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamesema radi hiyo iliwapiga wakati wakikusanya vifaa vyao ili warudi nyumbani.
