
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Philip Mpango, amekemea kuwepo Kwa watumishi ambao si waajiriwa ndani ya Mamlaka za Maji (vishoka) wanaoendelea kuchafua Wizara na Mamlaka za Maji, kwani ndio wanawaunganishia maji wananchi bila kufuata utaratibu na kusababisha malalamiko mengi na baadhi ya maeneo kukosa huduma hiyo.
.
Mhe.Mpango amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2021/2022 iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, ambapo pia amezitaka Mamlaka hizo kuacha kufanya kazi kwa mazoea ikiwemo kuzoea matatizo ya wateja na hivyo kutotimiza majukumu yao kwa ufanisi.