
Rais wa Kenya William Ruto, amesema maandamano ya kila wiki yanayoandaliwa na upinzani hayatasuluhisha matatizo yanayowakumba Wakenya, ikiwemo gharama ya juu ya maisha ambapo amemtaka kiongozi wa upinzani nchini humo, Raila Odinga ampe nafasi ili atekeleze aliyowaahidi Wakenya kwenye kampeni.
.
Ruto ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kaunti ya Kisii katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu kwenye eneo hilo ambapo pia amebainisha kuwa ana imani atamshinda Odinga katika kiny’anganyiro cha uchaguzi wa urais cha mwaka wa 2027.
