
Kufuatia kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mahakama imeshindwa kusikiliza mashauri ya watuhumiwa wa ugaidi kwa sababu ya kukosa bajeti, Mahakama hiyo imebainisha kuwa taarifa hizo si za kweli na zinalenga kupotosha.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mahakama imeeleza kuwa, suala la Bajeti haliwezi kuhusishwa na Mahakama, kwani bajeti ya kuita mashahidi inasimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na sio Mahakama.

