
Watu 6 wakiwemo watendaji wa serikali, wenyeviti wa vijiji na wananchi wasiokuwa waadilifu, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara, kwa kosa la kuiba mahindi tani 13, yaliyotolewa na serikali ili kupunguza makali ya bei, kisha kuyauza kwa wafanyabiashara.
.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bi.Mariam Chaurembo, ambapo amebainisha kuwa watu hao watafikishwa mahakamani kutokana na uhalifu huo.
