Back to top

URASIMISHAJI ISIWE KISINGIZIO CHA KUNYANG'ANYA WANANCHI VIWANJA

27 March 2023
Share

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Pinda, amewataka maafisa wa sekta ya ardhi kutotumia Urasimishaji kama kisingizio cha kunyanga'anya wananchi viwanja vyao jambo ambalo linazalisha migogoro.

Mhe.Pinda amekuja na maelekezo hayo baada ya kupokea malalamiko mengi ya wananchi ambao walikuwa wanamiliki maeneo makubwa, lakini wakati wa urasimishaji wamedai kunyang'anywa sehemu ya viwanja vyao.

Naibu Waziri Pinda ameeleza hayo mkoani Katavi na baada ya kukutana na watumishi wa sekta ya ardhi, mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya na watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo amepokea taarifa za utendaji kazi pamoja na kutoa maelekezo.

Aidha Naibu Waziri Pinda ametaka wananchi ambao wameisha kamilisha taratibu za umilikishwaji wapewe hati zao za kumiliki ardhi bila kuchelewa wala kusubiri wale ambao hawajakamilisha taratibu.