
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili, imeutaarifu umma kuwa majeruhi pekee wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea Februari 22, 2023, mkoani Dar es Salaam, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka Hospitali baada ya afya yake kuimarika, huku ikibainisha kuwa majeruhi huyo alipokelewa akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A.
.
Hata hivyo Bw.Milanzi ataendelea na huduma kama mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili.
