
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), nchini Kenya, Noordin Haji, ameondoa kesi za viongozi 6 wa upinzani walioshiriki kwenye maandamano yalioanziashwa na upinzani nchini humo.
.
Mkurugenzi huyo amefanya maamuzi hayo siku moja baada ya Rais wa nchi hiyo, William Ruto kumtaka Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga kusitisha maandamano ili kupisha njia ya Mazungumzo kuhusu madai yao.
.
Muda mfupi baadae Kiongozi huyo wa Upinzani alikubali na kusitisha maandamano hayo, yaliyokuwa yaendelee leo Aprili 03, 2023, ambapo nae alitaka kusimamishwa mara moja kukamatwa kwa viongozi waliohusika kwenye maandamano.
