Back to top

TAIFA LINAKABILIWA NA UMASIKINI WA KIPATO

03 April 2023
Share


Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Mpango, amesema bado taifa linakabiliwa na kiwango kikubwa cha umasikini wa kipato miongoni mwa Watanzania na baadhi ya mikoa ikitajwa kuendelea kuongoza kwa lishe duni, na udumavu licha ya kuwa katika kiwango kizuri cha  ukuaji wa uchumi.

Mhe.Dkt.Philip Mpango amaeyasema hayo Jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,  ambapo pia amezungumzia tatizo la  utofauti miongoni mwa Watanzania.

Awali, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba, amesema uwepo wa dira hiyo, utaweza kuleta matokeo chanya kwa taifa.

Amesema serikali imejipanga kuhakikisha dira hiyo inatekelezwa kwa vitendo katika ngazi mbalimbali.

Baadhi ya wadau walioshiriki katika uzinduzi wa dira hiyo wakiwemo wabunge, wamekiri kuwa dira hiyo inaonesha mwelekeo wa taifa kupiga hatua katika maswala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.