
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu, amesema mgonjwa mmoja wa Marburg mwenye umri wa miaka 26 ameruhusiwa akiwa na afya njema, ambapo ameitaka jamii impokee na kushirikiana nae katika shughuli zake.
.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo mkoani Dar es Salaam, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Marburg ulioripotiwa katika Wilaya ya Bukoba vijijini mkoani kagera mnamo Machi 21, 2023.
.
Waziri amesema kuwa jumla ya watu 212 waliotengamana na wagonjwa wamebainishwa na kati ya hao watu 35 wamemaliza siku 21 za uangalizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa huo.
