Back to top

WANNE WAFARIKI BAADA MCHUNGAJI KUWAAMBIA WAFUNGE HADI KUFA

14 April 2023
Share

Watu wanne wamefariki huku wengine zaidi ya 10 wakilazwa katika hospitali ya Kaunti ya Kilifi nchini Kenya, ambapo Polisi nchini humo wamesema watu hao walipatikana katika msitu waliokuwa wakiishi kwa siku kadhaa baada ya kuambiwa na Mchungaji wao, kufunga bila kula hadi kufa.
.
Mchungaji huyo aliyejulikana kwa jina la Paul Makenzie Nthenge wa Kanisa la Good News International, aliachiwa huru kwa dhamana ya polisi mwezi uliopita (Machi 2023) baada ya kuhusishwa na vifo vya watoto wawili waliodaiwa kufa kwa njaa ambao wazazi wao ni miongoni mwa wafuasi wake.