
Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi, ameagiza mishahara ya wafanyakazi wa Serikali ya mwezi Aprili, ifanyike mapema, kuanzia Aprili 14, 2023, kwa ajili ya matayarisho ya sikukuu ya Eid El Fitr ambapo hatua hiyo imelenga kuwapa muda wa kutosha wafanyakazi hao kufanya maandalizi ya sherehe hizo.
.
Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya siku ya Ijumaa, Aprili 21, 2023 au Jumamosi, Aprili 21, 2023, kutokana na kuandama kwa mwezi.
