Back to top

MELI YENYE WATALII 715 YATIA NANGA, DAR ES SALAAM

17 April 2023
Share

 Meli kubwa yenye watalii 715, iliyoanza safari yake kutoka nchini Marekani ikiwa na raia wa mataifa mbalimbali ya ikiwemo ya Ulaya, imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam ikitokea Zanzibar.
.
Watalii hao wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ikiwemo Makumbusho ya Taifa, Kijiji cha Makumbusho na soko la vinyago lililopo Mwenge na viwanja vya mnazi mmoja.


Ujio wa meli hiyo unatokana na jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini ambapo jitihada hizo zimeendelea kuzaa matunda.