Back to top

TANZANIA YATOA TAMKO VITA NCHINI SUDAN

18 April 2023
Share

Tanzania imetoa tamko la kulaani mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan ambapo Jeshi rasmi la nchi hiyo linapigana na Kikosi cha Kijeshi cha RSF kugombea madaraka. 
.
Tanzania imetoa tamko hilo kama Mwanachama wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ambapo imesema mapigano hayo yanasababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali unaorudisha nyuma maendeleo ya Sudan.
.
Katika Tamko hilo Tanzania huku imezitaka pande zote mbili kusitisha mapigano hayo na kuingia kwenye mazungumzo bila masharti ili kutafuta suluhisho kwa njia ya amani.
.
Aidha, Tanzania imesema iko tayari kusaidia juhudi za Jumuiya za kimataifa katika kutafuta amani ya kudumu nchini Sudan.