Back to top

MARUFUKU KUWEKA TINTED KWENYE SCHOOL BUS

19 April 2023
Share

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, mkoani Songwe, limepiga marufuku mabasi ya yanayotumika kubeba wanafunzi (School Bus) kuwa na vioo vinavyozuia kuona ndani (Tinted) ambayo yametajwa kuwa kichaka na chanzo cha vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa wanafunzi.
.
Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, SSP Joseph Bukombe, wakati wa ukaguzi wa magari hayo, zoezi lililoanza leo, ambapo magari 2 kati kati ya 14, yaliyokaguliwa yamezuiwa kutoa huduma baada ya kukosa sifa.