Back to top

RIPOTI CAG : MSIWE NA HOFU SERIKALI INACHUKUA HATUA

20 April 2023
Share

Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw.Gerson Msigwa, amesema wananchi wasiwe na hofu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kwani serikali inaifanyia kazi ripoti hiyo na itachukua hatua stahiki za kisheria kwa wale wote waliohusika kwenye ripoti hiyo.
.
Msigwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, ambapo amewatahadharisha wananchi juu ya upotoshaji wa ripoti hiyo.