Back to top

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KURUHUSU KULAWITIWA

20 April 2023
Share

Mahakama ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, imemuhukumu Tonny Kurwa(18), Mkazi wa Misungwi, mkoani Mwanza, kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuruhusu kuingiliwa kinyume cha maumbile.
.
Hukumu hiyo ya jinai namba 91/2023 imetolewa baada ya mshitakiwa huyo kukiri kutenda kosa hilo, ambapo alikuwa akitumia mbinu ya kuvaa gauni na sidiria na kujichanganya kwenye maeneo ya walevi (vilabu vya pombe).
.
Tony alitenda kosa hilo Aprili 12, 2023, huko maeneo ya klabu cha Songambele kilichopo wilaya ya Mbarali kinyume na kifungu namba 154 (1) (C) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
.
Mshitakiwa baada ya kusomewa shitaka lake alikiri kutenda kosa ndipo hukumu ilitolewa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama yake.