
Mkuu wa wilaya ya Rorya, Bw.Juma Chikoka ametoa siku 7 kwa uongozi wa shule ya msingi Ngasaro, kuanza ujenzi wa matundu 24 ya vyoo, baada ya shule hiyo kupewa fedha zaidi ya shilingi mil. 53, lakini ujenzi huo haujaanza.
.
Bw.Chikoka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wanafunzi na walimu katika shule hiyo kwenye wa zoezi la ugawaji wa madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB ambapo amebainisha kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa endapo ujenzi huo hautaanza.
