Back to top

SERIKALI YAJENGA NYUMBA 52 MWAKA WA FEDHA 2022/23

25 April 2023
Share

Serikali imejenga nyumba za Watumishi 52 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 3,417,556,981 katika hospitali za Rufaa za Mikoa na Hospitali za Kanda katika mwaka wa fedha 2022/2023, ikiwa ni sehemu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Bungeni jiji Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa serikali itaendelea na uboreshaji huo ikiwemo kuajiri Wataalamu wa afya na kuwahamisha Madaktari Bingwa kulingana na mzigo wa wagonjwa katika kituo husika.