
Olivia Naserian, anadaiwa kumuua binti yake aliyejulikana kwa jina la Glory Njeri, mwenye umri wa miaka miwili kwa kumkata vipande vipande kwa kisu, kisha kula sehemu za viungo vyake vya ndani.
.
Naserian anadaiwa kufanya unyama huo, kwenye makazi yake yaliyopo, eneo la Milimani Estate, nchini Kenya, siku ya Jumapili, kisha kumlaza ndani mtoto huyo, kabla ya majirani kutoa taarifa Polisi, ambao walifika eneo la tukio na kumkamata.
.
Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Kajiado nchini humo, ambapo Hakimu Mkuu, Jane Kamau ameamuru, Naserian abaki chini ya kizuizi cha Polisi kwa siku 10 nyingine ili kuruhusu maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi wao.
