
Serikali inakamilisha mapitio ya miundo ya kada za afya, ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2023, na itawasilishwa kwenye Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala na Bora kwa ajili ya kupata idhini, ili watumishi wa waanze kunufaika kutokana na maboresho hayo.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel, bungeni jijini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa miundo hiyo itawasaidia wataalamu mbalimbali wa afya, wakiwemo madaktari bingwa na wataalamu wengine waliopata fursa ya kujiendeleza katika kada zao.
