
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), mkoani Mbeya, kimewasimamisha kazi Mwenyekiti na Katibu wa Chama hicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, ili kupisha uchunguzi wa malalamiko ya wanachama kuhusu viongozi hao kutokomea na fedha za posho na chakula cha wajumbe walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), ambayo kimkoa yalifanyika kwenye uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya.
