Back to top

THBUB KUFANYA UCHUNGUZI HURU KIFO CHA NUSURA

10 May 2023
Share

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB), imeazimia kufanya uchunguzi huru, kufuatia kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Nusura Hassan Abdallah na ajali iliyomuhusisha Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt.Festo Dugange, baada ya Tume hiyo kubaini uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa haki za binadamu.
.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, huku akibainisha kuwa kumekuwa na kukinzana kwa taarifa baina ya vyombo vinavyotoa taarifa likiwemo Jeshi la Polisi.