Back to top

SITASAHAU MAUAJI YA ASKARI 9 KIBITI - SIRRO

10 May 2023
Share

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Mstaafu, Balozi Simon Sirro, amesema katika utumishi wake atakumbuka mambo Mengi ambayo yalimuumiza kichwa ikiwemo la kuuawa kwa askari 9, katika eneo la Kibiti , mkoani Pwani.
.
Balozi Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye hafla ya kumuaga iliyofanyika leo Mei 10, 2023, kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Taaluma ya polisi, kilichopo Kurasini ,mkoani Dar es Salaam.