Back to top

WIZARA YATOA NENO GHARAMA YA KUSAFISHA FIGO.

15 May 2023
Share

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amelieleza bunge kuwa serikali inaangalia uwezekano wa kupunguza gharama za matibabu ya kusafisha figo, katika Hospitali za serikali kutoka shilingi 350,000 na kufikia shilingi Laki 150,000 mpaka elfu 90,000.

Naibu Waziri Mollel, ameyasema hayo wakati akijibu swali bungeni, kuhusu serikali kupunguza gharama za kusafisha Figo ili wagonjwa wenye kipato cha chini waweze kumudu.

Hata hivyo amesema kwa sasa upo Utaratibu wa mgonjwa kufuata, ili kupata msamaha wa matibabu hayo ya kusafisha figo, endapo hana uwezo wa kumudu gharama hizo ikiwa ni pamoja na kupata barua ya uthibitisho kutoka mtendaji wa kata.

Kwa sasa huduma za kusafisha Figo zinapatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hospitali za Rufaa za Kanda na mikoa na hospitali maaalum ikiwemo ya Chuo Kikuu cha Dodoma.