Back to top

ITV YAPEWA TUZO YA ARIEL HEART OF GOLD

15 May 2023
Share

Rais wa Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF), amekitunuku tuzo ya Ariel Heart of Gold, Kituo cha runinga cha ITV, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa kituo hiki katika kuandaa maudhui yanayohusu utoaji wa elimu juu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu na Virusi Vya Ukimwi hapa nchini.

PICHA: Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhaville (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko ITV, Joyce Luhanga (wa kwanza kushoto) wakipokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais wa Taasisi EGPAF, Bi. Yolanda Brignoni (wa pili kutoka kulia) na Mwakilishi Mkazi wa EGPAF Tanzania, Dkt. Sajida Kimambo (wa kwanza kulia)


Tuzo hiyo imekabidhiwa na Makamu wa Rais wa Taasisi hiyo yenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, Bi. Yolanda Brignoni (wa pili kutoka kulia), ambaye aliambatana na Mwakilishi Mkazi wa EGPAF Tanzania, Dkt. Sajida Kimambo (wa kwanza kulia) na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhaville (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko ITV, Joyce Luhanga (wa kwanza kushoto).