Back to top

TANESCO YAJITOA, HITILAFU YA UMEME BUNGENI

15 May 2023
Share

Kufuatia kutokea kwa hitilafu ya umeme kwenye ukumbi wa Bunge na kusababisha vipindi vya Bunge kuahirishwa, Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limesema, baada ya ukaguzi kwa kushirikiana na wataalamu wa TAMESA pamoja Bunge walibaini kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na miundombinu iliyopo ndani ya kumbi za Bunge kwani laini inayohudumia upande wa Bunge haikuwa na changamoto.
.
Kupitia taarifa hiyo, Shirika hilo limesema wataalamu wake kwa kushirikiana na TAMESA pamoja na Bunge walifanikiwa kutatua changamoto iliyojitokeza na huduma ya umeme ndani ya Bunge ikarejea.