Back to top

Aliyemlazimisha mtoto kula kinyesi akamatwa Uganda

16 May 2023
Share

Polisi nchini Uganda wamemkamata mwanamke Esther Nabirye (26) aliyeonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni ikionyesha akimlazimisha mtoto wake wa kambo wa miaka minne kula kinyesi chake baada ya mtoto huyo kujisaidia kwenye kibaraza (veranda).

Akithibitisha kukamatwa kwake, Msemaji wa Polisi Fred Enanga amesema kuwa Nabirye tayari yuko chini ya ulinzi wa polisi na mashtaka ya kuteswa kwa watoto yamefunguliwa dhidi yake.

Aidha aliwapongeza majirani ambao walikuwa wepesi wa kumrekodi mwanamke huyo, ambapo pia amebainisha kuwa wanaamini kuwa kunaweza kuwa na ukatili mwingine uliokithiri dhidi ya mtoto huyo na wanachunguza suala hilo.

Pia alihakikisha kuwa mtoto huyo mdogo atapelekwa kwenye hifadhi ya dharura ambapo atapata huduma muhimu.