
Serikali mkoani Mtwara imesema matukio 693 ya ukatili dhidi ya watoto yameripotiwa mkoani humo kati ya Januari 2022 na Machi 2023 na makosa yaliyoongoza ni ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas, amesema hayo wakati akifungua kongamano la familia lililofanyika mkoani Mtwara lililodhuriwa na zaidi ya washiriki ya 300.
Amesema zaidi ya matukio 400 yaliwahusu watoto wa kike na 273 yaliwahusu watoto wa kiume.
Amesema matukio yaliyoongoza yalikuwa ya ukatili wa kijinsia ambayo yalikuwa 272, wakati matukio ya kingono yaliyoripotiwa yalikuwa 165 na ya kutelekezwa yalikuwa 147.
Kongamano hilo limeandaliwa na serikali ya mkoa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali.
