
Waziri Mkuu Mhe.Kasim Majaliwa ameunda tume ya watu 14 ambao Watazunguka nchi nzima, kuzungumza na wafanyabiashara pamoja wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya biashara na ameagiza ndani ya siku 14 tume hiyo iwe imemaliza kazi na mapendekezo yao yawe yamefikishwa serikalini kabla ya kikao cha bunge la bajeti hakijaisha.
Kwenye tume hiyo wajumbe 7 kutoka upande wa wafanyabiashara na wengine 7 kutoka taasisi za Serikali, ambao watapitia malalamiko yaliyotolewa kwa uwazi na wafanyabiashara kwa Waziri Mkuu, kwenye mkutano uliofanyika kwenye Uwanja wa Mnazi Mmoja.


Tume hiyo imepewa muda wa kuzunguka mikoani pamoja na Zanzibar na kuja na suluhisho la matatizo yaliyotolewa na wafanyabiashara.
Waziri Mkuu Majaliwa ametangaza kusimamishwa mara moja, Sheria mpya ya kodi ya maghala na Askari Polisi wametakiwa kuacha kutumika katika kukamata watu kuhusu stakabadhi.
Wafanyabiashara wamemhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa kuwa watafungua maduka yao.
