Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, amewatembelea wafugaji waliopo Kijiji cha Loliondo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Siku 3 mkoani Arusha na Manyara.
Katika Ziara hiyo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.David Silinde amewahakikishia wafugaji wa eneo hilo kuwa Wizara hiyo itaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha wafugaji wote nchini, na kuwataka kuendelea kufuga kisasa ili kuepukana na migogoro baina yao na watumiaji wengine wa Ardhi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (katikati) akijibu hoja mbalimbali za wafugaji wa kijiji cha Loliondo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) iliyofanyika kijijini hapo Meo 17, 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa kwenye mavazi ya kiongozi wa kabila la wasonjo mara baada ya kuvikwa nafasi hiyo na wafugaji waliopo eneo hilo wakati wa Ziara yake aliyoifanya kijiji cha Longido Mei 17, 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde muda mfupi baada ya kufika kwenye Uwanja wa ndege wa mkoa wa Arusha Mei 17,2023 ambako pamoja na mambo mengine alitembelea na kukagua shughuli za ufugaji mkoani humo na Manyara.