
Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa, 7% ya watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo, ambapo ametoa rai kwa wananchi kupima ugonjwa huo mara kwa mara ili kuepuka madhara kuwa makubwa zaidi, ikiwemo gharama ya matibabu ya ugonjwa huo.
.
Dkt.Mollel ameyasema hayo, Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mhe.Asia Halamga ambapo amebainisha kuwa katika kujali afya za Watanzania wakiwemo wenye ugonjwa wa figo, Serikali imetoa kiasi cha shilingi Bil. 290.9 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali za mikoa, vikiwemo vya matibabu ya kusafisha damu (dialysis) kwa wagonjwa wa figo.
