Back to top

ZITTO NA MWAROBAINI WA GHARAMA ZA MASHA

07 June 2023
Share

 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Bw.Zitto Kabwe ameishauri serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Chakuka kununua chakula kingi zaidi na kukihifadhi ukiwemo mpunga, ili kukiingiza sokoni wakati bei za vyakula ziko juu, ili wananchi wapate chakula kwa gharama nafuu na kumudu kuendesha familia zao wakati wa mlipuko wa njaa.

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Bw.Zitto Kabwe ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Doroth Semu, ameishauri serikali kurudisha kikokotoo cha awali kwa kuwa kikokotoo cha sasa hakina maslahi kwa watumishi.

ZITTO NA MWAROBAINI WA GHARAMA ZA MAISHA