Back to top

MAREKANI YASITISHA MSAADA WA CHAKULA ETHIOPIA

09 June 2023
Share

Marekani imesitisha msaada wa chakula kwa Ethiopia kwa sababu michango hiyo haiwafikii wale wanaohitaji.

Kauli hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Misaada la Marekani (USAid) limeeleza uchunguzi umebaini mpango unaendeshwa visivyo, hivy wameamua kufanya uamuzi mgumu lakini muhimu kwamba hatuwezi kusonga mbele na usambazaji wa msaada wa chakula hadi mageuzi yatakapofanywa.

Shirika hilo halijasema ni nani anayehusika na kampeni hiyo, lakini waraka wa taarifa za ndani ulionukuliwa na shirika la habari la Reuters unadai kuwa baadhi ya maafisa wanafanya hivyo kwa kutumia 'vitengo vya kijeshi kote nchini'.

Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa misaada ya kibinadamu kwa Ethiopia, ambapo zaidi ya watu milioni 20 wanahitaji msaada wa chakula, kwa sababu ya ukame na vita vya hivi majuzi katika eneo la Kaskazini la Tigray.

#Bbcswahili