Back to top

WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI AJALINI RUVUMA

12 June 2023
Share

Watu watatu wa familia moja wamefariki baada gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 864 EAV lililokuwa likitokea Madaba kuelekea Songea kugongana na gari la abiria aina ya Mitsubishi Rosa lenye namba za usajili T 186 DXM, katika eneo la Mliyayoyo, lililopo wilayani Namtumbo, mkoani Ruvuma.


Akizungumza na ITV, Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Marco Chilya, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Hilux, aliyehama upande wake na kuifata Mitsubishi Rosa.