
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Charles Mbuge, amesema wataendelea kuimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali katika kukabiliana na maafa ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika mazingira salama.
.
Meja Jenerali Mbuge ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha wataalam waliokutana kwa lengo la kuhuisha na kutafsiri mwongozo wa utekelezaji wa dhana ya afya moja kilichofanyika mkoani Singida, ambapo amesema mwongozo huo utarahisisha ushirikiano wa kisekta ili kujenga na kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya milipuko ya magonjwa na dharura zingine zenye madhara kwa afya ya binadamu, wanyama na mazingir
