
Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa, amewataka Makatibu Tawala wa Wilaya zote Tanzania Bara watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia utawala bora, miiko na maadili ya viongozi wa umma.
Ametoa maagizo hayo wakati akifungua semina elekezi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.
Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma katika maeneo yao na wanapobaini kuwepo kwa ubadhilifu wasisite kuchukua hatua.