Back to top

RMOS WASIMAMIENI WATUMISHI WASIKIUKE MIIKO

30 September 2023
Share

Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali Watu, Wizara ya Afya Dkt. Saitori Laizer, amewataka Waganga wakuu wa Mikoa nchini (RMOs), kuwajibika katika majukumu yao kwa kuwasimamia vyema watumishi wa Afya, ili kuhakikisha wanazingatia sheria na miiko ya kazi zao, kwani yeyote atakaekutwa na hatia ya kuvunja sheria au taratibu na miiko ya taaluma hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
.
Dkt. Laizer ameyasema hayo wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu kwenye kikao cha Baraza la Madaktari na Waganga Wakuu wa Mikoa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
.
Aidha, Dkt. Saitori amewataka Waganga hao kusimamia ubora wa Huduma za Afya na usalama wa wananchi wanapofika katika vituo vya kutolea Huduma hizo ili wapate huduma bora na kwa wakati.