
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limelaani idadi "ya kushangaza" ya watoto waliopoteza maisha huko Gaza, ambapo maafisa wanasema mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watoto 2,000.
Ripoti inasema kuwa watoto 2,360 wameuawa katika muda wa chini ya wiki tatu, huku ikotoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na upatikanaji endelevu na usiozuiliwa wa misaada ya kibinadamu.
"Watoto wengine 5,364 huko Gaza wamejeruhiwa katika "mashambulizi yasiyoisha,". UNICEF iliongeza.
Zaidi ya watoto 400 wanaripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kila siku katika eneo la Palestina lililozingirwa.
