Back to top

MSIWATISHIE WATOTO POLISI, WANAONA NI WATU WABAYA

19 January 2024
Share

Jeshi la Polisi, mkoani Tabora limewataka wananchi wenye tabia ya kuwatishia watoto wao pindi wanapokuwa wamefanya makosa kuwa watawaitia Polisi wawakamate, kuacha tabia hiyo kwani inajenga chuki dhidi ya Askari Polisi kwa watoto.
.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoani humo, Insp. Meshack Sanga, wakati akitoa elimu kwa jamii, juu ya madhara ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, ambapo amesisitiza kuwa hali hiyo huwajengea watoto uoga kwa Polisi na kuwafanya wakose haki zao za msingi kwa kuwaona Polisi ni watu wabaya.