Mason kuendelea kushikiliwa kwa unyanyasaji wa kingono.

Mchezaji wa soka wa Manchester United Mason Greenwood (20) aliyekamatwa siku ya Jumapili kwa tuhuma za ubakaji na shambulio ataendelea kuwekwa kizuizini kufuatia tuhuma zinazomkabili za unyanyasaji wa kingono na kutoa vitisho vya kuua.

Polisi wa Greater Manchester (GMP) walisema wamepewa muda zaidi wa kumhoji baada ya kuongezewa muda hapo awali hadi Jumatatu.

Manchester United imesema hatachezea klabu hiyo hadi itakapotangazwa tena.