Back to top

“Kombe la dunia lichezwe kila baada ya miaka miwili” Arsene Wenger

16 March 2021
Share

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa michuano ya kombe la dunia inatakiwa ichezwe kila baada ya miaka miwili kama ilivyo kwa michuano ya Ulaya EURO ili kuwapa nafasi wachezaji kushiriki tena na tena.
.
Arsene Wenger ambaye kwasasa ni mkuu wa kitengo cha maendeleo ya soka duniani kilicho chini ya FIFA ambaye pia ni mshauri wa karibu wa Rais wa FIFA Giann Infantino amesema kuwa michuano hiyo kuchezwa kila baada ya miaka minne sio sawa kwa wachezaji na michuano hiyo lazima ibebe maana kwa wachezaji kama ilivyo michuano ya Ulaya ya EURO.
.
Wenger amenukuliwa akisema kuwa..."Kama ukiangalia katika timu zinazoshiriki michuano ya kombe la dunia wastani wa umri kwa wachezaji unakuwa katika miaka 27 na 28, hivyo kwanini kwasababu michuano hiyo inafanyika kila baada ya miaka minne hivyo kunakuwa na nafasi finyu kwa wachezaji kurudi kuwania kombe hilo kama wamelikosa wakati husika kwani wakirudi katika michuano mingine watakuwa na wastani wa umri wa miaka 32 na 33".


"Hivyo ni Bora labda michuano hii iandaliwe kila baada ya miaka miwili kutoa nafasi kwa wachezaji" alisema Wenger 
.
Arsene Wenger amesema kuwa moja kati ya hoja itakayojadiliwa kwenye kikao chao cha mwezi huu ni kupunguza tarehe za mapumziko ya FIFA katika kalenda yao kwa ajili ya timu kufuzu michuano hiyo mikubwa duniani.
.
Wenger amesema kuwa hiyo itakuwa ni suluhisho la kujadili kurahisisha namna ya kufuzu kuliko kurudi tena Octoba, Novemba, Septemba kisha March na June lakini mpango huu kutawapa nafasi wachezaji kwa mwezi March na June kuvitumikia vilabu vyao.
.
Arsene Wenge pia amesema hawezi kupingana na wazo lake la kutaka kurudi katika kazi ya ukocha isipokuwa amekuwa na kazi nyingi za FIFA.