Back to top

Abiria wasio vaa barakoa kwenye vyombo vya usafiri kushushwa.

12 August 2021
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Amos Makalla amesema abiria ambao watakutwa kwenye chombo cha usafiri wa umma bila kuvaa barakoa watashushwa, lengo likiwa ni kupambana na wimbi la tatu la Corona.

Ameeleza kuwa utafanyika ukaguzi ambapo ukiwa kwenye Daladala, Mabasi yaendayo mikoani, Vivuko vya majini na Mabasi ya Mwendokasi kama hujavaa barakoa utashushwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Amos Makalla.