Back to top

ACT WAZALENDO YATAKA UCHUNGUZI KIFO CHA ENOCK

17 November 2023
Share

Chama cha ACT Wazalendo, kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillius Wambura, kuunda tume ya makamishna wa jeshi hilo kwa ajili ya kuchunguza kifo cha utata cha mfanyabiashara Enock Elias, Mkazi wa Kijiji cha Ilabiro Kata ya Katanga, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma  ambaye ameuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa kwenye mikono ya polisi na maafisa wa idara ya uahamiaji wilayani Kakonko.
 
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwenge wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe.Zitto Kabwe, amesema hatua hiyo itasaidia familia ya kijana huyo kupata haki na kujua chanzo cha kifo chake.