Back to top

AMUUA MWANAE KWA KIPIGO KISA KAIBA KUKU WAWILI

28 November 2023
Share

Douglas Tendwa, mwenye umri wa miaka 36, mkazi wa Kakamega nchini Kenya anashikiliwa na Polisi nchini humo, akituhumiwa kumpiga hadi kumuua mwanae wa kiume aliyejulikana kwa jina la Shadrach Luseno mwenye umri wa miaka 13, baada ya kuiba kuku wawili kisha kuondoka nyumbani kwa muda siku nne.
.
Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 26 majira ya saa 11 jioni, ambapo mtoto huyo alipoteza fahamu kutokana na kipigo kisha kupelekwa hospitali ambako madaktari walisema kuwa tayari amefariki.