
Wakala wa huduma za misitu wilaya ya Bagamoyo mkoni Pwani (TFS) wamekamata basi la abiria lenye namba za uisajiri T612 DFU likiwa limebeba mkaa zaidi ya gunia 25 kinyume na taratibu zilizowekwa.
Basi hilo ambalo ufanya safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Mazinde mkoani Tanga limekamatwa katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu kilichopo Sanzale wilaya ya Bagamoyo baada ya maafisa wa wakala wa huduma za misitu nchini kuendesha zoezi la ukaguzi katika barabara ya Msata Bagamoyo.
Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri na basi hilo wamelalamikia baadhi ya mabasi kubeba mikaa kinyume cha sheria kwa lengo la kukwepa kodi na kuomba serikali kuendelea na msako pamoja na kuwachukulia hatua sitaiki.
Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Bagamoyo Mkaguzi msaidizi wa polisi Azizi Zuberi amesema kitendo cha kupakia mkaa kwenye basi la abiria ni miongoni mwa makosa hatarishi katika suala la usalama wa barabarani huku akiwataka madereva kuzingatia sheria zilizowekwa ili kuepuka usumbufu pindi wakikamatwa.